Mabingwa wa nchi watambulishwa bungeni
DODOMA; VIONGOZI na wachezaji wa Klabu ya Yanga wametambulishwa bungeni leo walipohudhuria vikao vya bunge kwa mwaliko rasmi wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro.
Dk Ndumbaro aliwaalika wachezaji na viongozi wa klabu hiyo wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2024/25 bungeni mjini Dodoma leo.