Mabomu baridi kudhibiti tembo
DODOMA; WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na JWTZ imeboresha kilipuzi (bomu baridi) kwa ajili ya kudhibiti tembo wanapoingia kwenye maeneo ya wananchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki, amesema bomu hilo lilizinduliwa rasmi Mei 13, 2024 na baada ya uzinduzi tarehe 22 Mei 2024 wizara ilikabidhiwa rasmi mabomu baridi 4,000 katika Makao Makuu ya Shirika la Mzinga-Morogoro kwa ajili ya kuanza kutumika kwenye halmashauri 20 zilizo katika mifumo ikolojia 5 Nchini.
“Halmashauri za wilaya hizo ni pamoja na Nachingwea, Liwale, Manispaa ya Lindi (Mchinga), Mtama, Ruangwa, Tunduru, Namtumbo, Karatu, Same, Mwanga, Mvomero, Mkinga, Korogwe, Meatu, Busega, Itilima, Bariadi, Bunda Mjini, Bunda Vijijini na Karagwe.
“Zoezi hili litaendelea katika maeneo mengine yenye changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu,” amesema.