Mabondia wajitosa kutangaza utalii
DAR ES SALAAM: WACHEZAJI wa Masubwi wameingia rasmi kutangaza utalii kupitia mchezo wa ngumi kupitia Pambano la ‘sisi kwa sisi’ linalotarajia kufanyika Novemba 25, 2023 jijini Arusha
Kupitia mchezo huo bondia Abdallah Pazi maarufu kama “Dulla mbabe anatarajiwa kuzichapa na Bondia kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema Leo Oktoba 23, 2023 Promota wa pambano hilo kutoka Kampuni ya Lady in red Sophia Mwakagenda amesema lengo la Pambano hilo ni kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
“Pambano hili ni kwa ajili ya kutangaza utalii wa ndani, ndiyo maana tumepeleka Arusha lakini kuendeleza vipaji vya vijana wetu kutokana na ukubwa wa mabondia ambao wanacheza siku hiyo utalii wetu utazidi kufahamika nje ya mipaka ya Nchi yetu,”amesema Mwakagenda.
Pia amesema pamoja na Pambano hilo kutakuwa na mapambano mawili ya wanawake kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao katika masumbwi.
Hata hivyo bondia Dullah Mbabe amesema amejipanga vyema kuhakikisha analipiza kisasi kutoka kwa mpinzani wake, Erick Katompa.
“Nilikuwa nataka pambano kati yangu na bondia Katompa kabla ya mwaka kuisha ili tuweze kumaliza kisasi chetu hii sasa ndio fursa kwangu na mashabiki wangu.”
“Kuona nalipa kisasi hiki Arusha na hii ni kwa mara ya kwanza nitaenda kutembelea vivutio vya utalii na fursa ya kipekee kama mzalendo kutangaza Utalii kama alivyofanya Rais Samia Suluhu kupitia Filamu ya “Royal tour “amesema
Mabondia wengine pia watapanda ulingoni ambao ni Shaban Kaoneka, Lauren Japhet, Jacob Maganga na wengine wengi.