Maboresho ya masoko Ubungo kuongeza mapato

WILAYA ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, imetakiwa kuangalia namna ya kuyaboresha masoko yake ili wananchi wapate eneo zuri la kupata mahitaji yao, pamoja na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.

Mkuu wa Wilaya hiyo,Hashim Komba amesema hayo wakati wa kikao cha kuwasilisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa Kamati ya Ushauri ya Wilaya Ubungo.

Komba amesema,” Eneo la Malamba mawili pale wafanya biashara wanapofanya biashara zao na namna
lilivyozidiwa maana yake kule bidhaa zao zinauzika.

“Tuangalie namna gani tutaliboresha badala ya kuwatoa wafanyabiashara na kuwapeleka eneo lingine kwa kuwa pale tayari kuna biashara. Halmashauri itapata mapato,” amesema.

Ameshauri pia maeneo mengine ya masoko Shekilango na Sinza Makaburini, halmashauri iyaangalie, ijiwekee lengo kwenye bajeti ijayo ifanye nini.

Mkurugemzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ubungo, Elias Ntiruhungwa amesema karibu asilimia 90 katika masoko waliyonayo hayanufaishi manispaa.

Amesema mwaka ujao wa fedha wajitahidi hilo tatizo wahakikishe wanalimaliza.

Habari Zifananazo

Back to top button