Maboresho yaanza Uwanja Lake Tanganyika

CHAMA Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, kimesema kuwa uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma umeanza kufanyiwa maboresho, ili kuruhusu michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iweze kufanyika.

Katibu wa chama hicho, Omari Gindi amethibitisha kuanza kwa maboresho kwenye uwanja huo ambao unatumiwa na timu ya Mashujaa iliyopanda Ligi Kuu Tanzania Bara na iitautumia kama uwanja wake wa nyumbani.

Ametaja maeneo ambayo ukarabati huo unafanyika ni pamoja na kujengwa kwa ukuta ambao ulidondoka, kuweka paa kwenye baadhi ya maeneo ya jukwaa la Mashariki na Magharibi, ujenzi wa vyoo vya mashabiki, maboresho ya vyumba vya kubadilishia na mifumo ya maji.

Advertisement

Kwa upande wake Meneja wa uwanja huo, Shaban Buti alisema kuwa ukarabati wa maeneo mbalimbali ya uwanja yanaenda vizur,i ikiwemo eneo la kuchezea (pitch) kwa kuondoa majani yasiyotakiwa, kumwagilia maji na kuweka nyasi kwenye usawa unaotakiwa.

2 comments

Comments are closed.

/* */