Mabula: Wadau saidieni timu za wanawake

MBUNGE wa jimbo la Ilemela Dk Angeline Mabula amewaomba wadau mbalimbali wa soka mkoani Mwanza kujitokeza kwa wingi katika kuzisaidia timu za wanawake Mkoa wa Mwanza na kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Dk Mabula amesema hayo leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Chama cha Soka la wanawake mkoa wa Mwanza (WFAMZ) uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Amekipongeza chama cha soka cha wanawake mkoa wa Mwanza kupitisha katiba yao.

Advertisement

‘’Tunapanda na kushuka kwenye soka kwa sababu wadau hawajawa na ukaribu na michezo na kuona umuhimu wa kuchangia ili kuweza kuzisaidia timu zetu ziweze kufanya vyema’’ amesema Dk Mabula.

Mwenyekiti wa chama hicho Sophia Makilagi alisema bado hali ya soka la wanawake sio nzuri

‘’Bado hali ya soka la Wanawake kwa Sasa siyo nzuri, tuna timu Moja Ligi Kuu (Alliance girls), na tatu daraja la kwanza (Bilo academy,Ukerewe queens na TSC Academy)’’ amesema Makilagi.

Amesema katika ligi ya mkoa wa kuna timu Tatu za Marsh, Jona, Sandumina na Chuo Kikuu cha mtakatifu Agustino( SAUT).

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *