Macvoice atamani kujiunga WCB

MSANII chipukizi na anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Macvoice amesema kuwa iwapo itatokea nafasi ya kwenda kujiunga na lebo ya WCB yuko tayari kama Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ watafikia makubaliano.

Macvoice ambaye hivi sasa yuko chini ya lebo ya Next Level chini ya Mkurugenzi wake, Rayvanny, ambaye ndiye aliyempa nafasi ya kuonesha kipaji chake, anaamini bado ana safari ndefu kwenye muziki wake.

Alisema kuwa muziki ni biashara, hivyo yeye hawezi kukataa kufanya kazi na WCB ambayo ni miongoni mwa lebo kubwa hapa nchini na barani Afrika ambayo imewainua wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva.

“Siwezi kuikataa ofa hiyo kwani mimi bado ni mjukuu wa Diamond Platnumz na kama utaratibu utafuatwa hakuna kitu ambacho kitashindikana katika kukamilisha hili,” alisema Macvoice.

Alisema kuwa ndoto yake ya kufika mbali kimuziki kama kutakuwa na nafasi ya kumvusha kumfikisha mbali zaidi ya hapo kwani malengo yake ni kuutangaza muziki wake kimataifa, hili litafanikiwa iwapo ataendelea kuwa kwenye mikono salama kama alipo hivi sasa.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button