Madaktari bingwa kutoka Marekani wawasili nchini

MADAKTARI bingwa 60 wa mifupa na nyongo kutoka Los Angeles, Marekani wamewasili Arusha na kuanza kazi katika Hospital ya Rufaa ya Selian inayomilikiwa na Kanisa na Kiinjili Tanzania (KKKT) Kanda ya Kaskazini.

Kauli mbiu ya ujio wa madaktari hao ni ‘’Upendo wa Mama Rais Samia suluhu Hassan kwa Wananchi wake’’.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospital ya Selian,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospital hiyo,Dk Godwin Kivuyo alisema ujio huo ambao ni mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan ni faraja kwa hospital hiyo na wagonjwa wote nchini wa magonjwa ya mifupa na nyonga.

Dk Kivuyo alisema kuwa wagonjwa 400 walikwenda katika hospital hiyo wakikabiliwa na ugonjwa wa mifupa na nyonga na huenda idadi hiyo isipate matibabu kwani wanaweza kupata matibabu wagonjwa wasiopungua 50 kwa madaktari hao wa Kimarekani.

Alisema hospital hiyo ilianza kufanya upasuaji wa magonjwa ya mifupa na nyonga tangu Machi mwaka huu na hadi sasa wagonjwa 200 wameshapata tiba katika hospital hiyo kabla ya madaktari bingwa kufika katika hospital hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema ujio wa madaktari hao unaweza kusaidia fursa mbalimbali kwa madaktari wa hapa nchini

‘’Ninamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaalika madaktari hao kuja nchini kwa ajili ya kutoa tiba bure kwa wagonjwa wa mifupa na nyonga moyo huo unapaswa kupongezwa kwa dhati.” alisema Dk Kivuyo

Kivuyo alisema mbali ya kufanya huduma hiyo ya upasuaji bure kwa wakazi wa jiji la Arusha na nje ya jiji hilo kwa magonjwa  magoti na nyonga pia watakuwa wakitoa mafuzo kwa madaktari bingwa wa Hospitali ya Selian katika shughuli za upasuaji.

Mkurugenzi Kivuyo alisema kuwa wagonjwa watakaopata huduma ya upasuaji wa magoti na nyonga kwa madaktari hao bingwa kutoka Marekani ni wale tu wenye uwezo wa hali ya chini kwani ndio walengwa wakubwa.

Lazaro Nyalandu mdau wa afya na mratibu wa ujio wa madaktari hao alisema lengo lake ni kutaka huduma hiyo kwenda katika kanda zote nchini ili wagonjwa wa mifupa na nyonga waweze kupata huduma hiyo bure.

Nyalandu alisema muda wa wiki mbili waliopata madaktari hao ni mchache ila wakati mwingine watapanga uataratibu ili wagonjwa waliokuwa maeneo mengine waweze kupata huduma hiyo na hiyo yote inafanyika kwa baraka za Rais samia Suluhu Hassan .

Alisema Rais aliweza kuwaalika madaktari hao kuja nchini kwa ajili ya kutoa matibabu hayo bure kwani watanzania wenye hali ya chini hawawezi kugharamia matibabu hayo kwa kuwa ni ghali kwani matibabu ya mgonjwa mmoja aliyefanyiwa upasuaji na madaktari hao ni dola 30,000.

Mratibu huyo alisema kuwa mbali ya kufanya upasuaji pia watakuwa wakifanya somo darasa kwa madaktari wa Hospital ya Seliani ili kupata uelewa zaidi ya upasuaji wa magoti na nyonga na hiyo ni fursa kwa madaktari wa Kitanzania waliopo katika hospitali hiyo.

Nyalandu pamoja na kuishukuru sana serikali na Rais Samia kwa ushirikiano waliouonyesha na wageni hao kwa kanisa la KKKT pia wanatarajia kuwaleta madaktari bingwa wa akima mama kutoka Marekani kufanya tiba bure.

Habari Zifananazo

Back to top button