Madaktari Ivory Coast kuamua hatima ya Pacome

JANGWANI, Dar es Salaam: HATIMA ya nyota wa Yanga SC, Pacome Zouzoua bado ni kizungumkuti baada ya Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe kutanabahisha kuwa jukumu la afya ya mchezaji huyo kwa sasa halipo mikononi mwao.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, Kamwe amesema taarifa za awali za Pacome Zouzoua zinaeleza kuwa ameumia goti, lakini baadae zikaja taarifa za kuitwa timu ya taifa hivyo taarifa kamili zitatolewa na madaktari wa timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo mawasiliano kati yao ni ya karibu.

Kuhusu majeruhi wengine kikosini Kamwe amesema “hali ya Wachezaji wetu ambao walipata majeraha Kibwana Shomari ataanza mazoezi mepesi hivi karibuni, auchokhalidofficial anaendelea na sehemu ya pili ya mazoezi.

Advertisement

Gift Mauya hali yake imeimarika.

Yaokouassi Attohoula alichanika nyama za paja na hali yake ni 50/50 kuelekea mchezo wetu wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi Mamaelodi.” Amesema Kamwe.