Madaktari wafutiwa leseni ukiukaji maadili

BARAZA la Madaktari Tanganyika (MCT) limewafungia leseni madaktari 16 na kufutia leseni watoa huduma wanne kwa kipindi cha mwaka 2023 kutokana na makosa mbalimbali ya kitaalum baada ya kukiuka maadili.

Baraza hilo pia lilitoa onyo wataalamu 14 ambao walibainika kwenda kinyume na maadili.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jiji Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa baraza hilo Prof David Ngassapa alisema kati ya Januari 22 hadi 26,2023 walisikiliza jumla ya mashauri tisa yanayohusisha ukiukwaji wa kanuni za maadili na utendaji wa kitaaluma na kutoa maamuzi.

“Wanataalum waliopewa adhabu mbalimba ni 33 kuna walifutiwa leseni,kuna waliofungiwa leseni kwa muda na kuna waliopewa onyo kali kutokana na kukiuka maadili ya kitaalama ,”ameeleza.

Amesema wanataalum hao waliofungiwa leseni wamefungiwa kuanzi kipindi cha miezi sita hadi miaka miwili na kupewa maelekezo tofauti tofauti kulingana na makosa yao ikiwemo kulipa fidia.

Amesema kwa mwaka 2023 baraza imesikiliza jumla ya kesi 11 na kutolea maamuzi kwa kipindi cha mwezi Januari 23 hadi 27 ambapo mashauri 10 yakisikilizwa Agosti 7 hadi 12,2023.

“Aidha katika mashuri haya pande zote mbili b zilifahamishwa na haki ya kukata rufaa kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 43(2),(3) na 44 cha sheria ya udaktari ,udaktari wa meno na afya shirikishi.

Prof Ngassapa ametoa rai kwa wanataaluma kuzingatia kanuni na maadili ya kitaaluma za mwaka 2005 na kufuata muongozo wa watoa huduma kwa lengo la kulinda afya ya mgonjwa.

Amesema baraza linaelekeza kuzingatiwa kwa misingi ya maadili ikiwemo kujaza fumo ya ridhaa ya huduma kwa wagonjwa ,kumuelimisha mgonjwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na tiba inayotolewa na njia mbadala ya matibabu endapo itahitajika.

“Mengine ni Mwanataaluma kuhakikisha hachunguzi mgonjwa akiwa mwenyewe bila mtaalamu mwingine wa kusaidia ,kurekodiwa na kuhifadhiwa kwa taarifa za wagonjwa kwa kufuata taratibu,wanataaluma kuhakikisha wanafanya na wanatumia majibu ya vipimo kwenye kutoa tiba kulingana na miongozo .

Amesema ni muhimu wataalamu wasimamizi kwenye maeneo ya kazi wahakikishe wanaona wagonjwa kwa muda muafaka na kusimamia kazi zinazotekelezwa na wanataaluma walioko chini yao.

“Baraza halitawavumia wanataaluma ambao hawafuati misingi ya maadili katika utendaji wao wa kazi ,baraza linatoa wito kwa mamlaka zinazosimamia utendaji kazi kuhakikisha wanafanya usimamizi wa ndani na wan je na ukaguzi wa huduma zinazotolewa kwa wagonjwa ili kubaini changamoto zao.

Habari Zifananazo

Back to top button