Madanguro 320 yagundulika Kinondoni

WILAYA ya Kinondoni imeyagundua madanguro 320, kwa mujibu wa Mstahiki Meya, Songolo Mnyonge.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mnyonge alisema madanguro 150 yapo Mwananyamala, 135 Tandale na 35 Msasani na kwamba wamepanga kuyateketeza.

Katika kuhakikisha wanakomesha biashara hiyo, Mnyonge amesema vita waliyoianzisha ni endelelevu hatua ya kwanza walioifanya ni kukusanya taarifa za maeneo yanayofanya biashara hizo.

“Hatua ya pili tutawaita mwenyenyumba wote ambao shughuli hizi zinafanyika. Ukipewa kiwanja kinaeleza ni makazi, kama ni biashara kuna biashara zimehainishwa kwa sababu ukienda kwenye nyumba, maeneo mengi unakuta nyumba zimebadilishwa.” Alisema Mnyonge.

Amesema kama wananchi wakiiunga mkono kampeni hiyo, basi watafanikiwa kuimaliza biashara hiyo kwa kuwa watu wengi wanaipinga kwa kuwa inaiharibu jamii yetu na nikinyume cha sheria.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button