Madarasa 100 sekondari kujengwa Arusha

Madarasa 100 sekondari kujengwa Arusha

SERIKALI ya Rais Samia Suluhu Hassan, imetoa Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 100 katika shule za sekondari 20 jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na kutoa miezi miwili na nusu kwa wakuu wa shule kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo.

Pia Mkuu huyo wa wilaya, ameagiza kamati za ujenzi zishirikishwe, ili kuhakikisha fedha zinatumika ipasavyo na kutoa angalizo kwa wakuu wa shule watakaocheza na fedha hizo watachukuliwa hatua ikiwemo kuvuliwa madaraka yao.

Advertisement

“Fedha hizi ni za serikali mkizichezea au kuchelewesha ujenzi huu wa madarasa mtawajibika, ikiwemo kuwapeleka Takukuru,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Hargeney Chitukulo,  amesema fedha hizo zitajenga madarasa 100, ili kuwezesha wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwakani wasikose vyumba vya madarasa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *