Madarasa 134 sekondari kujengwa Mtwara

Mtwara waanza maandalizi uzinduzi wa Mwenge

SERIKALI imetoa Sh bilioni 2.680 kwa ajili ya ujenzi vyumba vya madarasa 134 kwa shule za sekondari katika Mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema ujenzi wa madarasa hayo ni kwa ajili ya matayarisho ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.

“Fedha zimeshafika na Halmashauri wameshazipokea na wameanza utekelezaji, ili ifikapo Januari mwaka 2023 wanafunzi waweze kuingia kwenye vyumba vilivyokamili, vikiwa na madawati,” amesema.

Advertisement

Amesema ujenzi wa vyumba hivyo, vinatakiwa kujengwa na kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu, huku akizitaka Halmashauri na ngazi zote zinazohusika katika ujenzi huo kuzingatia utaratibu unaotakiwa katika ujenzi wa madarasa hayo.

Amewataka wasimamizi  kuhakikisha ujenzi unazingatia thamani ya fedha, huku akionya watakaoenda kinyume na utaratibu wa ujenzi wa madarasa hayo.

“Kwa yeyote akayeenda kinyume na utaratibu unaotakiwa tutashughulika naye, kwa sababu hatuko tayari kuona fedha nyingi kama hizi zinachezewa, halafu tunafika mwisho fedha zimeisha, miradi haijaisha,” amesema.