ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Yanga, Iman Omary Madega atazikwa leo wilayani Chalinze mkoani Pwani.
Madega alifariki jana akiwa katika Hospitali ya Msoga wilayani humo. Madega aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.
Hata hivyo taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga jana ilieleza kuguswa na msiba huo na kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Aidha, Simba katika taarifa yao kwenda kwa umma wameungana na Yanga kuomboleza msiba huo.