Madereva 1,522 wakiuka sheria za barabarani

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata madereva 1,522 wa magari, bajaji  na pikipiki kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Alex Mkama amesema hayo  leo Juni 26, 2023  wakati akitoa taarifa kuhusu  operesheni mbalimbali zilizofanyika mkoani humo kwa kipindi cha Juni 1, mwaka huu hadi Juni 26, 2023.

Amesema miongoni mwa madareva hao , 305 waliamriwa kwenda shule za mafunzo ya udereva na wanaendelea na mafunzo hayo, ili waweze kupata leseni .

Alisema, madereva  234 walielekezwa kununua kofia ngumu na walifanya hivyo ,  madereva 1,502 waliandikiwa faini kwa mujibu wa sheria na wengine 20 walifikishwa  mahakamani.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button