Madereva safari za usiku kuthibitishwa

MAMLAKA ya Udhibiti Usafi ri Ardhini (Latra), imesema itatekeleza agizo la serikali la kuondoa zuio la safari za usiku kwa kudhibiti mifumo ya vidhibiti mwendo isichezewe, sambamba na kuthibitisha madereva wa safari hizo ili kuhakikisha usalama wa abiria.

Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habib Suluo alibainisha hayo mkoani Dar es Salaam alipozungumza na HabariLEO jana akieleza watakavyotekeleza agizo hilo.

Alisema watashirikiana na Jeshi la Polisi kujua ni maeneo gani wataanza nayo kulingana na hali ya barabara na usalama uliopo.

“Tutashirikiana na polisi kwa sababu wao ndio wanaokuwa barabarani, tutakubaliana tuanze wapi, hatuwezi kuanza nchi nzima kwa sababu tayari kuna maeneo waliyatolea tahadhari,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ramadhani Ng’anzi alitaja maeneo hayo kuwa ni Pori la Burigi, Pori la Katavi na mabasi yanayokwenda Mkoa wa Kigoma ambapo mabasi hayataruhusiwa kuendelea na safari kama yatafika Mkoa wa Tabora saa 6 usiku.

Suluo alisema moja ya vitu ambavyo viliishawishi serikali kuondoa zuio hilo ilikuwa ni uwepo wa mfumo wa vidhibiti mwendo (VTS), unaoratibiwa na Latra lakini mamlaka hiyo imegundua udanganyifu unaofanywa na madereva wa mabasi na wakati mwingine wakishirikiana na baadhi ya wamiliki wasio waaminifu.

Alisema Latra imegundua kuwa wapo madereva wanaochezea mfumo kwa kuzima vifaa hivyo wanapokuwa safarini kisha kwenda mwendo kasi huku wakisingizia kukosekana mtandao bila kujua kuwa mifumo ya Latra inatunza kumbukumbu za nyuma.

“Wanakwambia ni mtandao lakini sisi teknolojia tunayotumia ni ya satelaiti, inatunza kumbukumbu za nyuma kwa hiyo wanapowasha inatupa kumbukumbu zilizopita na hata wanapochezea waya au kutoa betri, mfumo unatupa taarifa kuwa betri imetolewa, kuna taarifa sisi tunapata wao hawapati,” alisema Suluo.

Alisema kwa sasa Latra inashughulikia suala hilo na kuhakikisha linakomeshwa na ikiwa kuna dereva yeyote ataendelea na mchezo huo basi lake litafutiwa ratiba ya usiku na halitaruhusiwa tena. Alisema kwa sasa Latra.

Habari Zifananazo

Back to top button