Madereva School Bus wadaiwa kunajisi watoto

WILAYA ya Kinondoni imenzisha utaratibu wa kuweka Matron katika gari za kubeba wanafunzi kutokana na kuibuka kwa vitendo vya ubakaji kwa watoto vinavyodaiwa kufanywa na madereva.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na walezi, wakidai watoto wao kufanyiwa vitendo vya ubakaji katika magari hayo ya shule.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Maofisa Ustawi wa Jamii nchini, Gondwe aliwataka wazazi na walezi kuwa makini kufuatilia taarifa za watoto na kujenga ukaribu, ili wanapokumbana na changamoto waseme haraka.

“School Bus mtoto anapanda wa kwanza anashuka wa mwisho na bahati mbaya wazazi hawafuatilii watoto, hivi karibuni kuna mama alikuja kulalamika mwanaye alifanyiwa ukatili.

“Dereva alipaki gari akaenda kumfanyia mtoto shambulio la kikatili na mtoto alivyofika nyumbani alikuwa huru kuzungumza na mama,” ameeleza.

Amesema mtoto huyo waligundua amefanyiwa ukatili, wakati anaogeshwa, ambapo alikuwa anapata maumivu, baada ya kuulizwa alisema dereva alimfanyia ukatili.

“Kesi ziko nyingi watoto kufanyiwa ukatili kwenye School Bus, tusiwaamini sana hiyo ni changmoto,  kwenye mabasi Kinondoni tumesema lazima awepo matron na tumepitisha hiyo sheria,” amesisitiza.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x