MADEREVA wametakiwa kutii sheria za usalama barabarani huku ikielezwa asilimia kubwa ya ajali zinatokana na harakati za kulipita gari jingine ‘overtake’.
Hayo yamesemwa Jana na Meneja wa Kitengo cha Usalama Barabarani kutoka makao makuu ambapo alisema alama za barabarani madereva wengi wamekuwa hawazitii kutokana na uzembe.
Daffa alisema mwendokasi kwa madereva pia unachangia ajali michoro imechorwa ambayo inaonyesha uendelevu, kuna kona kali lakini dereva anang’ang’ania kutoka nje ya michoro huku akiwa mwendokasi unao hatarisha.
“Tanroads imefanya juhudi za kupunguza ajali kwa kuweka alama za barabarani ambapo imekuwepo changamoto ya alama za kugongwa au kuibiwa nondo zilizosimikwa barabarani.”alisema Daffa.
Mtaalamu kutoka kitengo cha mizani makao makuu Tanroads, Vicent Tarimo amesema kufuatia sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya udhibiti uzito wa magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 ambazo zimeanza kutumika hapa nchini mwezi Machi mwaka 2019.
“Uzito uliopitiliza katika gari ni chanzo pia cha watu kupata ajali hivyo wananchi wanatakiwa wakiona hali hiyo watoe taarifa ili kuweza kuokoa maisha yao kwani yapo magari yanayobeba abiria yakiwa na mzigo uliopitiliza uzito”alisema Tarimo.
Tarimo amesema magari yenye uzito wa kuanzia 4.5 yanatakiwa yapite mizani na Ile desturi ya gari kujaza abiria na kuwafaulisha pembeni kukwepa mizani watu hao wakibainika wachukuliwe Sheria.