Madereva wakumbushwa kufuata sheria Arusha

WAMILIKI wa vyombo vya usafirishaji jijini Arusha, daladala na bajaji wametakiwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na serikali katika usafirishaji abiria vinginevyo dola haitawaacha salama.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafirishaji Ardhini (LATRA) Mkoa wa Arusha, Joseph Michael katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kutoa elimu ya kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri.

Meneja huyo alisema wamiliki wa vyombo vya usafiri wanapaswa kufuata sheria za barabarani ikiwemo kwenda katika njia walizopangiwa, kushusha abiria katika vituo vilivyopangwa ,na wanapaswa kuwa na leseni iliyotolewa na LATRA vinginevyo hatua kali zitachukuliwa.

Aidha amesema kuwa bajaji zote zenye leseni zimeelekezwa sehemu ya maegesho hivyo vyombo hivyo vyote vinapaswa kufuata sheria na barabara ya Sokoine ‘hiace’ na bajaji haziruhusiwi kupita nyakati zote na zikikutwa sheria itachukuliwa.

Meneja huyo alisema kabla ya kuanza kwa njia mpya kwa vyombo hivyo, elimu kwa umma ilifanyika ikiwa ni pamoja na jamii kujua njia mpya ili kuondoa usumbufu usikuwa na sababu kwa jamii na hilo limefanyika kwa kusimamiwa na LATRA.

Alisema na kutoa onyo kwa kwa vyombo visivyokuwa na leseni ya LATRA katika kufanya biashara ya usafiri Arusha kuwa mamlaka hiyo haitawaacha salama kwani hatua kali zitachakuliwa dhidi ya madereva wakaidi ikiwa ni pamoja na kuwafungulia mashitaka mahakamani.

‘’Nasisitiza hiace na bajaji zinapaswa kuwa na leseni ya LATRA na kama huna utakamatwa tu hivyo ofisini yangu inafanya kazi masaa 24 kila mmiliki anapaswa kukata leseni na kufuata taratibi alizopangiwa na sio vinginevyo.’’ alisema Michael

Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha ,Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (RTO) ,Zauda Momamed amesema changamoto zote zilizotolewa na wamilikiwa daladala dhidi ya polisi zitafanyiwa kazi ili wamiliki hao waweze kufanya kazi kwa usalama.

Mohamed alisema kuwa lengo kuu ni kutaka wamiliki wa daladala na madereva wao kufanya kazi kwa kufuata sheria za usalama barabarani kwani ndio siri ya kuepuka ajali zisizokuwa na maana wakiwa na vyombo vya usafiri.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
KathyNelson
KathyNelson
2 months ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by KathyNelson
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x