Madiwani Mpimbwe wahoji ujenzi wa barabara

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoa wa Katavi, limemtaka Meneja wa wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kuhakikisha anashughulikia barabara zote zinazotakiwa kutengenezwa.

Wakichangia taarifa ya utekelezaji wa barabara iliyowasilishwa na Meneja wa TARURA Wilaya ya Mlele, Mhandisi Maneno Makorongo juu ya ukarabati wa barabara za halmashauri hiyo, madiwani wamesema inasikitisha kuona barabara zinashindwa kukamilika kukamilika kwa wakati na nyingine hata hazijaanza ujenzi.

Awali akitoa ufafanuzi, Mhandisi Makorongo amesema tatizo la kuchelewa kukarabatiwa barabara hizo ni changamoto ya uhaba wa wakandarasi, jambo ambalo lilipingwa na Mwenyeketi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Sailas Irumba.

“Kila siku mkandarasi, mkandarasi.

Meneja sisi hatutaki hao wakandarasi, nchi hii ina wakandarasi wengi tunataka wananchi wetu Halmashauri ya Mpimbwe waweze kuneemeka na fedha anayoitoa Mheshimiwa Rais kwenye TARURA,”amesema.

Baada ya Mwenyekiti kutoa kauli hiyo, Mhandisi Makorongo aliwaahidi madiwani kuwa atazingatia ushauri uliotolewa na kuufanyia kazi.

Habari Zifananazo

Back to top button