MADIWANI wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelalamikia kushindwa kufanyika shughuli za maendeleo katika robo mbili za mwaka kutokana na mfumo wa kuhamisha fedha kushindwa kufunguka.
Madiwani hao ambao ni diwani kutoka kata ya Kisuke Joseph Bundala na diwani kutoka kata kinamapuka Samweli Sharifu wametoa hoja hiyo leo tarehe 16/Novemba/2022 katika kikao Cha baraza la madiwani.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Doa Limbe amesema wamekuwa wakihitaji maendeleo lakini suala la mfumo limeonekana kukwamisha na liko nje ya uwezo wa halmashauri.
Mhasibu wa halmashauri hiyo Prosper Mlacha amesema hakuna mfumo wa halmashauri ya Ushetu bali mfumo huo unatumika kwa nchi nzima na unasimamiwa na Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi).
Naye ofisa mipango wa halmashauri hiyo Theresa Ndumba amesema kweli shughuli za maendeleo zimesimama sababu ya mfumo kutofunguka lakini tayari wametenga sh Millioni 440 kwaajili ya kutekeleza miradi.