Madiwani watakiwa kudhibiti wizi wa fedha za miradi

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kusimamia miradi mbalimbali inayofanyika kwenye halmashauri zao ili kudhibiti wizi ya fedha

Mongella ametoa agizo hilo leo wakati wa kujadili hoja za CAG kwa mwaka 2022/23 katika hiyo iliyopata hati inayoridhisha.

Amesema zaidi ya Sh milioni 300 hazijakusanywa kieletroniki (POS) na kupelekea halmashauri hiyo kulalamika hakuna hela ilhali fedha hizo zimeliwa na walioteuliwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Advertisement

Ametoa mfano geti la Engaruka Sh milioni 7 hazijawekwa benki na Sh milioni 9 hazipelekwa benki katika geti la mto wa mbu na kuagiza kuwa lazima sasa halmashauri hiyo ikusanye fedha kwa njia za kieletroniki na kupelekwa benki.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Happiness Laizer amesisitiza kuongeza kasi ya usimamizi wa fedha hizo ili waweze kupata maendeleo kwani kiuhalisia Halmashauri hiyo inafedha nyingi zisizopelekwa benki.

Aliahidi ushirikiano baina ya madiwani hao na wakuu wa idara katika kuhakikisha fedha zinazoletwa katika halmashauri hiyo zinatumika ipasayo katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa wananchi.

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *