Madiwani watakiwa kufuatilia miradi ya maendeleo

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ametoa rai kwa madiwani wa halmashauri ya Karatu kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao  pamoja na kamati ya fedha na uongozi kufanya ziara za kukagua miradi mara kwa mara.

Mongella ametoa agizo hilo wilayani Karatu, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha za kupitia utekelezaji wa hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu  na Serikali za Mitaa(LAAC)kwa mwaka wa fedha 2021/23.

Amesisitiza madiwani hao ni lazima wasimamie miradi ya maendeleo, kwani kuna miradi mingi viporo haijakamilika katika kata zao, ili wananchi waweze kupata maendeleo.

Amesema moja ya miradi ambayo imeshindikana kukamilika licha ya kuletewa fedha na serikali kuu ni maradi wa kituo cha afya cha mbuga nyekundu, ambacho kililetewa Sh milioni 500, lakini mpaka sasa hakijakamilika licha ya kuongezewa fedha bado milango iliyowekwa imepasuka.

“Kuna miradi kichefuchefu ukiwemo mradi wa mbuga nyekundu, ambayo milango ya kituo cha afya imepasuka pasuka, lakini fedha zimekuja nyingi na mradi haujakamilika mpaka sasa licha ya serikali kuu kuleta fedha za kutosha,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button