Madrid, Man City mechi ya kisasi

MADRID, Hispania; Real Madrid leo watakuwa wenyeji wa Manchester City katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mchezo huo unatizamwa zaidi na wapenda kandanda ulimwenguni kutokana na upinzani ulioneshwa na timu hizo zilipokutana michezo iliyopita.

Manchester City iliitupa nje Madrid katika michuano ya msimu uliopita kwa kuifunga jumla ya mabao 5-1 kwenye michezo miwili ya Nusu Fainali.

Winga wa Real Madrid Vinicious Junior amenukuliwa akisema huu ndio muda wa timu yao kulipa kisasi kwani wana timu bora ikilinganishwa na msimu jana.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameeleza kuwa licha ya kufahamu ubora wa wapinzani wake dhamira yake ni kuwaachia maumivu Madrid wakiwa uwanja wao wa nyumbani na kisha kwenda kumaliza kazi nchini Uingereza.

Kwenye michezo 10 ya mwisho miamba hiyo ilipokutana Manchester City imeshinda michezo minne, Real Madrid ikisajili ushindi mara tatu huku zikipatikana sare tatu.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button