Maeneo yenye migogoro kufanyiwa uhakiki Katavi

SERIKALI itafanya uhakiki wa maeneo ya vijiji yenye muingiliano wa mipaka ambayo yanaonekana kuwa na migogoro ya ardhi mkoani Katavi.

Akizungumza baada ya kutembelea  baadhi ya maeneo hayo ikiwemo eneo la Visima Viwili lililopo katika Kata ya Kasekese wilayani Tanganyika, Mwenyeketi wa Kamati ya Mawaziri wa kisekta, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki,  amesema kuwa maeneo  yote yarejewe na  kufanyiwa tathimini upya.

Kutokana na hali hiyo, amewaomba wananchi kutoendelea kufanya makazi katika maeneo hayo.

Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta walianza ziara ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975, Jumanne Oktoba 11, 2022 katika Mkoa wa Rukwa, jana walikuwa Katavi na leo mkoani Kigoma.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x