Mafunzo ya pamoja ya Jeshi Tanzania na China yahitimishwa

PWANI: Mafunzo ya pamoja kati ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na jeshi la Jamhuri ya watu wa China yamefikia tamati Septemba 15 mkoani Pwani kwenye kituo cha CTC Mapinga.
Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha ulinzi na usalama kwa lengo la kupambana na ugaidi wanchi kavu na baharini, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili mwaka 1964.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Stergomena Tax amesema mafunzo hayo yanaimarisha uhusiano na mshikamano kwa pande zote mbili na kuongeza weledi na ukakamavu katika maeneo mbalimbali.
Pia amesema kwa upande wa teknolojia Jeshi litapiga hatua Kwa kutumia vifaa kama ndege ndogo zinazo ruka bila rubani ” Drons” Kwa kukusanya taarifa kwa weledi wa hali ya juu.
Balozi wa china nchini Tanzania Chen Mingjian amesema ‘’ napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mwenyeji wetu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ambao wameandaa vyema zoezi hili la pamoja, kuwakumbatia wanajeshi wa China kwa ukarimu, kuwatendea wema kama ndugu na jamaa, na kujitolea kikamilifu kwa urafiki.
Jumla ya wahitimu 151 wamehitimu mafunzo hayo ya pamoja na kutakiwa kudumisha yale waliyojifunza kwa kipindi cha wiki mbili.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button