Mafunzo ya sayansi kuongezea hamasa wanafunzi

SERIKALI kwa kushirikina na wafadhili wanatarajia kujenga vituo vya mafunzo ya sayansi kwa vitendo Ili kuongeza hamasa ya wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi na teknolojia wakiwa katika hatua za awali za masomo yao.

Vituo hivyo ambavyo Kwa sasa vipo katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam kwa kuanzia serikali inatarajia kujenga kituo kikubwa Dodoma na kuendelea katika mikoa mingine

Hayo yalisemwa na Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda wakati wa ziara yake katika kituo cha mafunzo ya sayansi Kwa vitendo Stemp park kilichopo Jijini Tanga.

Advertisement

Alisema kuwa uwepo wa vituo hivyo utasaidia kuongeza hamasa Kwa wanafunzi wengi kuweza kujifunza masomo ya sayansi Kwa njia rahisi na nyepesi yenye kuhamasisha ubunifu.

“Tunapokwendea hatuhitaji wanafunzi wakariri tuu notes zinazotolewa na Mwalimu darasani bali Kwa kutumia mafunzo Kwa vitendo aweze kuwa mbunifu mwenyewe Kwa kujifunza Kwa njia rahisi huku Mwalimu akibaki kuwa msimamizi tuu”alisema Waziri Mkenda

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  kituo cha Steam Park, Dk Lwidiko Mhamilawa  alisema kuwa kituo hicho kimeweza kuwa msaada mkubwa Kwa walimu kuweza kufundisha Kwa vitendo masomo ya sayansi.

 

“Mradi huu umesaidia kuongeza hamasa ya kusoma  masomo ya sayansi toka wakiwa wadogo katika nyanja ya teknolojia uhandisi na mahesabu kutokana na mwitikio wa wanafunzi wengi kutembea kituo hicho”alisema Dk Mhamilawa.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *