Mafuriko yaleta njaa Somalia

MAFURIKO nchini Somalia yaliyosababisha vifo vya watu 31, mpaka kufikia jana, yameleta shida ya ukosefu wa chakula.

Takribani watu milioni 1.6 wameathiriki na mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo kwa wiki mbili sasa.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ( OCHA ) imeeleza mafuriko yameshabishwa na mvua za El-Nino ambazo zinaendelea kuleta shida kwenye baadhi ya nchi duniani kote.

Rais wa Somalia, Hassan Mahamud amekiri kuwa changamoto yao kwa sasa ni uwepo wa njaa.

“Watu wamehama makazi yao, nyumba zimebomolewa, mali pia, watu wetu wamekumbwa na njaa na hii ndio changamoto yetu kwa sasa, tunaangalia namna ya kushughulika na haya.” amesema kiongozi huyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x