Mafuriko yaua 120 DR Congo

HABARI: Watu 120 wamefariki dunia kwa mafuriko katika Mji Mkuu wa Kinshasa nchini DR Congo. Taarifa nchini humo zinaeleza.

Taarifa ya Al Jazeera imefafanua kuwa wengi waliopoteza maisha walikuwa katika maeneo ya vilima ambayo yalikumbwa na maporomoko ya ardhi kutokana na mvua kubwa.

Vitongoji vyote vilifurika maji na matope, nyumba, barabara na visima vilibomolewa kutokana na maporomoko ya ardhi, ikiwa ni pamoja na barabara kuu ya N1 inayounganisha Kinshasa na Bandari Kuu ya Bahari ya Matadi.

Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza katika taarifa yake kwamba barabara hiyo inaweza kufungwa kwa muda wa siku nne. Serikali ya nchini hiyo imetangaza siku tatu ya maombolezo ya kitaifa inayoanza leo.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaohamia Kinshasa katika miaka ya hivi karibuni na jiji hilo linakabiliwa na upungufu wa mifereji ya maji na mipango duni ya miji.

Idadi ya waliofariki ilikusanywa na Usimamizi Mkuu wa Uhamiaji, sehemu ya wizara ya mambo ya ndani, na taraifa zinaeleza kuwa huenda ikaongezeka zaidi.

Waziri wa afya Jean-Jacques Mbungani Mbanda ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wizara hiyo imehesabu watu 141 waliofariki lakini idadi hiyo ilihitaji kuchunguzwa na idara nyingine.

Kinshasa ilipokuwa mkusanyiko wa vijiji vya wavuvi kwenye kingo za Mto Kongo, imekua mojawapo ya miji mikubwa barani Afrika yenye wakazi wapatao milioni 15.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button