Mafuriko yaua 13 Ufilipino

Mafuriko yaua 13 Ufilipino

VIFO vya watu vilivyotokana na mafuriko vimefikia 13 huku zaidi ya 45,000 wakiokolewa na kuhifadhiwa kwenye vituo maalumu, wengi waliopotea ikitaarifiwa ni wavuvi huko nchini Ufilipino.

Vifo hivyo vinajumujuisha mtoto wa mwaka mmoja na mzee wa miaka 64, eneo la kusini mwa Jimbo la Misamis. Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua ya siku mbili yameathiri watu 166,000

Advertisement

Mkuu wa shirika la maafa katika mji wa Clarin jimbo la Misamis Occidental, alikiambia kituo cha redio cha DZBB kwamba shughuli za uokoaji zinaendelea na pamoja na kuokoa baadhi ya maeneo yaliyokuwa na shughuli za kilimo.

“Uharibifu mkubwa hapa ni mifugo,” Meya wa mji wa Clarin Emeterio Roa alisema kwenye redio.

Ofisi ya hali ya hewa ya nchi hiyo, Utawala wa Huduma za Anga ya Ufilipino, Jiofizikia na Unajimu (PAGASA), imesema  mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika maeneo ya nchi, na maporomoko ya ardhi yanayosababishwa na mvua kuna uwezekano katika baadhi ya maeneo yakaathirika zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *