WATU watatu wa familia moja wamefariki dunia miongoni mwao ni mwamanke mwenye umri wa 73 baada ya kusombwa na mafuriko ya maji ya mvua katika mto Mgolole eneo la mtaa wa Misongeni , Kata ya Bigwa , Manispaa ya Morogoro baada ya kunyesha kwa mvua kubwa .
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro , Shaaban Malugujo amesema tukio hilo la mafuriko na maji ya mvua kujaa na kusababisha athari hizo zilitokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia Janauri 10, 2024.
Aliwataja waliofariki na miili yao kupatikana ni mtoto Husnati Julius Thomas (6) na Theresia Adolf (73) wakati mwili wa Mwanahamisi Issa (35) ulikuwa haujapatikana na shughuli za utafutaji na uokoaji zilikuwa zinaendela.
Katika tukio hilo mtu mmoja akijiokoa baada yakusombwa na maji na kisha kushika mti kumwezesha kupanda juu na kukaa takribani saa nne hadi pale maji ya mvua yalipopungua nay eye kupata nafasi ya kutemka chini.
Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Morogoro , amemtaja katika tukio aliyenusurika na kujeruhiwa alitambuliwa kwa jina la Sengo Hamis (47).
Malungujo amesema , Sengo alijiokoa baada ya kufanya jitihada binafsi za kuweza kujiokoa kwa kukwea ( Kupanda ) juu ya mti mrefu na kukaa juu yake kwa muda mrefu hadi maji yalipopungua na kushuka chini.
Amesema miili ya watu wawili iliyopatikana ilishakabidhiwa na kwenda kuhifadhiwa Chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, wakati majeruhi huyo alipelekwa Hospitali ya masista ya Mgolole kwa matibabu zaidi.
Zeozi hilo la utafutaji mwili uliosalia litaendela kufanyika kwa uadilifu , kwa uwezo mkubwa na uelezi mkubwa ili kuweza kufanikisha kuuopoa mwili huo na kuweza kuwakabidhi wahusika .
“ Kwa taarifa za tukio hili zilifikia Jeshi la Zimamoto na Uakoaji majira ya saa 8: 17 asubuhi hapa unaweza kuona ukubwa wa muda uliokuwepo ambao unaweza kusababisha madhara kuwa makubwa” amesema“..
” kama taarifa hizi zingetolewa mapema zaidi , huwenda tungeweza kuhabatisha hata kuwapata wakiwa hai tofauti na huyu majeruhi ambaye amajinasua peke yake na pia huu mwili tunaoendelea kuutafuta tuneweza kuuona “ amesema Malungujo .
Mbali na tukio la Kata ya Bigwa, alitaja tukio lingine la mvua hizo ziliripotiwa katika eneo la Kata ya Kingolwira kwa kuhusishwa kuzingirwa kwa nyumba za makazi ya watu wanne na walifanikiwa kuwaokoa watu hao na wapo eneo salama .
Hivyo ametoa rai kwa wananchi katika kipindi hiki cha mvua zianzonesha na kutarajiwa kunyesha wajitahidi kukaa mbali na maji yanayotembea na wasiyapime kwa macho bali watembee na fimbo ndefu itakayowezesha kupima kina cha maji kabla ya kuvuka .
“ Usijaribu maji kwa kuyapima kwa miguu na hili ndilo lililosababisha kuwakuta hawa wenzetu waliopotenza maisha kulingana na taarifa za mashuhuda ambaye ni majeruhi aliyelazwa Hospitalini” amesema Malungujo.
Naye kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bigwa, Emmanuel Mamba amesema alipata taarifa ya tukio hilo saa kumi usiku na alifika eneo hilo ili kuhakiki hiyo nyumba na kuona imejengwa kwenye mkondo wa maji .
Mamba anasema walipojitahidi kuvuka kwenda kujisalimisha ng’ambo ya pili ya mto kwa bahati mbaya walisombwa na maji lakini baba aliweza kunusurika .
Amesema waliofariki ni wa familia moja kwa maana ya mtoto, mama mkwe na mke wa mwenye nyumba hiyo ambaye yeye aliweza kujiokoa baada ya kufanikiwa kupanda kwenye mti hatua chache baada ya kusombwa na maji hayo na kuweza kutoa taarifa hiyo.