Mafuriko yauwa watu 22 Dr Congo

MFAURIKO yaliyosababishwa na mvua kubwa katikati mwa DR Congo yamesababisha vifo vya takriban watu 22, wakiwemo 10 wa familia moja, afisa wa eneo hilo alisema.

Mvua iliyonyesha kwa saa moja katika Wilaya ya Kananga jimbo la Kasai ya Kati iliharibu nyumba na majengo mengi, gavana wa jimbo hilo, John Kabeya, alisema huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa ni ya mara kwa mara katika taifa hilo. Mwezi Mei, zaidi ya watu 400 walikufa katika mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha katika jimbo la Kivu Kusini Mashariki.

Habari Zifananazo

Back to top button