DAR ES SALAAM :MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeyafungia maghala mawili ya Mbolea ya Kampuni ya YARA yaliyopo mkoani Tabora na Mbeya.
Magala hayo ambayo yapo yamefungiwa baada ya kubaini Kampuni kufungasha mbolea iliyokwisha muda wake kwenye vifungashio vipya jambo ambalo ni kosa la kisheria.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa (TFRA) Joel Laurent amesema kutokana kosa hilo Mamlaka imesimamamisha shughuli zote za biashara za kampuni hiyo katika maeneo husika huku akitoa onyo kwa wafanyabiashara wa mbolea na wakulima watakaojaribu kufanya udanganyifu.
Nae, Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku Taifa Luis Kasela akizungumza amesema wataendelea kushughulikia wote wanaofanya udanganyifu na amewataka wafanyabiashara kutambua kuwa wataendelea kubaini kasoro na udanganyifu kwa kutumia njia za Kidgitali.
Hadi kufikia Desemba 31,2023 upatikanaji ulikuwa ni tani 797,871 sawa na asilimia 89 ya mahitaji ya mbolea kwa mwaka 2023/2024 ambayo ni tani 848,884.