Magani atenguliwa Halmashauri ya Korogwe

DOHA: RAIS Samia Suluhu Hassan Ametengua uteuzi wa Halfan H. Magani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe na badala yake kumteua Ndugu Goodluck Abinala Mwangomango.
Kabla ya uteuzi huu Ndugu Mwangomango alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.
Aidha Rais Amemteua Said Majaliwa kuwa Mkurugenzi wa Tanga Mjini. Kabla ya uteuzi huu Majaliwa alikuwa Mkurugenzi Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga.
Amemeteua Faraja Paschal Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kilindi Mkoani Tanga Kabla ya uteuzi huu Msigwa alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Amemteua Naima Bakari Chondo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida mjini Naima anachukua nafasi ya Goodluck Abinala Mwangomango ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe.
Pia Rais Samia, Amemteua Shamim Adam Sadiq kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa.
Amemteua Hamza Hussein Hamza kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Ngorongoro ambapo anachukua nafasi ya Nyakia Ally Chirukile ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.
Kabla ya uteuzi huu Hamza alikuwa Afisa Tarafa wa Ngudu, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.
Amemteua Lameck Karanga Ng’ang’a kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Ng’ang’a ambaye alikuwa Katibu Tarafa Karatu anachukua nafasi ya Msigwa aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilindi.
Amemteua Musa N.Kuji kuwa Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Shirikla Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA). Bw. Kuji alikuwa Naibu Kamishna wa Huduma za Shirika (TANAPA).