Magonjwa ya ngono chanzo cha matumizi holela ya Antibiotiki

DAR ES SALAAM: MAGONJWA ya ngono yametajwa kuwa chanzo cha matumizi holela ya dawa za antibiotiki nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, magonjwa ya ngono na homa ya ini.

Amesema, vitendo vya matumizi holela ya dawa za antibiotiki yameongezeka kutokana na hofu ya kunyanyapaliwa na kunyooshewa vidole kutoka kwa wahudumu wa afya.

“Wengi wanaona aibu kwenda hospitali kuonana na wataalamu wa afya kwa ajili ya vipimo, kutokana na kuogopa kunyanyapaliwa, lakini matumizi holela ya dawa tunatengeneza janga ambalo tutakuja kulia, usugu wa dawa utakuwa hautibiki,”amesema na kuongeza

“Juzi CMO (Mganga Mkuu wa Jiji) alikuwa ananiambia kuna aina moja ya dawa na nyie ni mashahidi.. matangazo kuhusu PID yamejaa. Maambukizi katika via vya uzazi yamejaa na dawa hadi zile supplements sijui ni kweli..!!! Embu mpango huu uweke mkazo kwenye elimu, tuwaelimishe watu sio kila PID inatibika kwa antibiotic moja,” amesema

Aidha, amesema magonjwa hayo yana uhusiano wa karibu na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani asilimia kubwa wanaogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ambao hawajaanza dawa wana magonjwa ya ngono.

Amesema utafiti uliofanyika mwaka 2016-17 umeonesha ugonjwa wa Kaswende ulikuwa mara tano zaidi kwa watu wenye virusi vya UKIMWI ukilinganisha na asilimia 0.8 na watu wasio na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Ameongeza kuwa wenye virusi vya UKIMWI walikuwa na dalili za kutokwa na uchafu na vidonda sehemu za siri kuliko wasio na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Takwimu zinaonyesha matumizi ya dawa dhidi ya vimelea nchini yanakadiriwa kufikia asilimia 62.3, sambamba na makadirio ya usugu kwa asilimia 59.8 huku utafiti ukionyesha wengi hutumia antibaotiki bila ushauri wa daktari.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) Moshi ulionyesha asilimia 92.3 ya wauzaji 82 walisambaza dawa hizo bila cheti cha dakktari mwaka 2017.

Utafiti huo wa mwaka 2021 zaidi ulionyesha kati ya watumiaji watumiaji 960 jijini Dar es salaam, asilimia 70.6 walijibu kwamba waliacha kutumia antibiotiki baada ya dozi kukamilika, na asilimia 42.3 hutumia iwapo zilibaki nyumbani au kwenda kununua ikiwa ndugu au rafiki zilimsaidia.

Utafiti huo ulibaini asilimia 57 kati ya wanafunzi 374 wa vyuo vikuu viwili vya Moshi walinunua wenyewe dawa bila ushauri wa daktari.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button