Magonjwa yasiyoambukiza tishio 2030

TAKWIMU za Wizara ya Afya zinaonesha kuwa katika kila vifo vitatu kifo kimoja kinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamebainishwa na waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo wakati akizindua kampeni ya uelimisha wa magonjwa yasiyoambukiza jijini Dar es Salaam.

Ummy amesema zamani watu walikuwa wanasubuliwa na malaria,kipindupindu, Tb kifaduro, ukimwi sasa magonjwa yasiyoambukiza yanakuja juu katika oridha ya takwimu.

Aidha ameainisha kuwa magonjwa mawili makuu ambayo ni shikizo la juu la Damu na kisukari yanachangia asilimia 70 ya magonjwa ya moyo ,figo na kiharusi.

“Kuna saratani ya shingo ya kizazi ni ya kwanza na saratani ya matiti inapanda kila wagonjwa 100 wa saratani wagonjwa 13 ni wa saratani ya matiti kwa kiasi kikubwa inakabili wanawake lakini hata wanaume asilimia moja wanapata saratani wataalamu wanasema inatibika ikiwahiwa mapema.

Amesema katika kupambana wanajikita katika magonjwa saba shikizo la juu la damu,kisukari,saratani ,kiharusi,sickle cell,macho,Afya ya akili na magonjwa ya ajali.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x