MAHAKAMA ya Juu nchini Kenya, imebariki ushindi wa William Ruto kuwa Rais wa nchi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya, uliofanyika Agosti 9, 2022.
Uamuzi huo umetolewa na mahakama hiyo muda mfupi uliopita, kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea urais kupitia Muungano wa Azimio, Raila Odinga aliyekuwa akilalamikia uadilifu katika uchaguzi huo, ambao Ruto aliibuka mshindi.