Mahakama Shinyanga kusikiliza kesi sita leo

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali ameanza kusikiliza mashauri ya kesi sita za mauaji kwa washtakiwa wanaotuhumiwa kutenda makosa hayo katika maeneo mbalimbali wilayani Kahama mkoani hapa.

Hayo yalisemwa Jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Edmund Kente alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alisema jaji Mahimbali atasikiza mashauri hayo ambayo upelelezi wake umekamilika .

Kente alisema mashauri hayo washtakiwa walidaiwa kutenda makosa hayo tangu mwaka 2021 ikiwa shauri moja limeanza kusikilizwa jana likiwa na mashahidi nane.

Advertisement

Kente alisema mashahidi sita jana walisikilizwa na leo mashahidi wawili wanaendelea kusikilizwa na jaji wa Kanda ya Shinyanga hadi hatua ya kuzitolea hukumu.

“Mashauri ya mauaji takwimu zake zimeenda zikipungua Ila ninatoa wito kwa wananchi wakiona Kuna viashiria vyovyote vya vitisho vitakavyopelekea mauaji watoe taarifa kwenye vyombo vya dola ili badaaye kuja kuisaidia mahakama.”alisema Kente.

Kente alisema kesi za mauaji ziko tofauti zenyewe kisheria zina ukomo wa muda wa upelelezi wao mahakama ya wilaya kupitia mahakimu waliopo wamekuwa wakizisikiliza na kuzitolea hukumu.

“Ninawashauri Wananchi wawe tayari kutoa ushahidi wa kweli kwani wapo mashahidi ambao wamekuwa wakipangwa na hawakushuhudia tukio hilo zinaleta usumbufu”alisema Kente.

Kente alisema kesi za mauaji hazina dhamana na upelelezi wake unakwenda taratibu pia mkemia wa serikali ambaye anathibitisha ofisi yake inazidiwa aliwaomba wananchi watii sheria zilizopo

5 comments

Comments are closed.