MAHAKAMA ya Kikatiba ya Thailand leo Agosti 24 imemsimamisha kazi Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha wakati ikitazamia shauri la kesi ambayo inaweza kumfanya kuondolewa madarakani siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.
Vyama vya upinzani vimewasilisha kesi ya kikatiba vikidai Prayuth, ambaye aliingia madarakani katika mapinduzi ya 2014, alikuwa amefikia kikomo chake cha miaka minane.
Taarifa ya mahakama ilisema majaji walikubali kwa kura 5 dhidi ya 4 kumsimamisha Prayuth hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.
“Mahakama ilizingatia ombi na nyaraka zilizowasilishwa zote zikiwa na hoja ya msingi na kwamba wana kesi ya msingi,” ilisema taarifa hiyo.
“Kwa hivyo, kura nyingi za [Prayuth] kusimamishwa kama waziri mkuu, kuanzia Agosti 24, 2022, hadi mahakama itatoa uamuzi.”
Hata hivyo, haku kuwa na tangazo la mara moja kuhusu nani angechukua majukumu ya Prayuth kama kaimu waziri mkuu.
Chini ya sheria za Thailand, Naibu Waziri Mkuu Prawit Wongsuwan, ambaye ameorodheshwa wa kwanza kati ya manaibu kadhaa, angetarajiwa kuchukua nafasi hiyo.
Prawit ni mmoja wa washirika wa karibu wa kisiasa wa Prayuth, anayetoka katika kundi lilelile la kijeshi lililoanzisha mapinduzi ya 2014 ambayo yalimuingiza madarakani.
Majaji watalazimika kuamua ni lini Prayuth alichukua mamlaka kikamilifu kuhusiana na katiba ya ufalme wa 2017, ambayo inamzuia waziri mkuu kuhudumu kwa zaidi ya miaka minane kwa jumla.