Mahakama yamuachia huru aliyehukumiwa miaka 30 kwa kubaka

K’NJARO; Moshi. MAHAKAMA Kuu Kanda ya Moshi, imemwachia huru na kumfutia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, mshitakiwa Nickas Lyimo aliyedaiwa kujaribu kumbaka mpwa wake (13).

Mahakama hiyo imemwachia mshitakiwa huyo kwa kigezo cha kukinzana kwa umri wa mlalamikaji ulionakiliwa kwenye hati ya mashitaka ni miaka 13, huku ushahidi uliotolewa na bibi wa mlalamikaji alidai mjukuu wake alikuwa na miaka 14.

Akisoma hukumu hiyo leo, Jaji Adrian Kilimi amesema kuwa Novemba 16, 2021 maeneo ya Kilema wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, mshitakiwa alifanya jaribio la kumbaka mjomba wake (13) kwa kumuingiza chooni na kumvua nguo kwa lengo la kumfanyia vitendo hivyo vya ukatili.

Amesema kuwa mshitakiwa alikana mashitaka yake na upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi wawili huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi wawili.

Ameeleza kuwa baada ya kusikiliza ushahidi huo Mahakama ya Wilaya ya Moshi ilimuhukumu kifungo cha miaka 30 jela.

“Mtoto huyu alikuwa anaishi na bibi yake ambapo siku ya tukio bibi alienda kwenye mazishi katika Kijiji cha Kimaroni na kumuacha mjukuu wake na mshitakiwa alikuja na kutaka kujaribu kumbaka hivyo, mtoto huyu alipiga kelele na mshitakiwa alikimbia,” amesema Jaji Kilimi.

Ameongeza kuwa mshitakiwa katika rufaa yake alidai kuna ukinzani kati ya ushahidi wa mlalamikaji na hati ya mashitaka kuhusu eneo lililofanyika tukio ambapo hati ya mashitaka inaeleza kuwa Kilema na mtoto akidai ni Kijiji cha Posho.

Jaji Kilimi amesisitiza kuwa; ” Upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka haya bila kuacha shaka hivyo, namfutia hatia na kifungo chake na naamuru aachiwe huru,” amesema Jaji Kilimi.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button