Mahakama yatoa ufafanuzi kesi za watuhumiwa ugaidi

MAHAKAMA ya Tanzania imekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mashauri ya watuhumiwa wa ugaidi hayajasikilizwa kwa sababu ya Mahakama kukosa bajeti.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Mahakama ya Tanzania, Artemony Vincent imeeleza kuwa hakuna kauli ya namna hiyo ambayo imetolewa na Jaji Mfawidhi au kiongozi mwingine yeyote wa Mahakama.

“Aidha, suala la bajeti haliwezi kuhusishwa na Mahakama kwani bajeti ya kuita mashahidi inasimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na sio Mahakama. “Kwa hiyo hata anayesambaza taarifa hizo haelewi mgawanyo ulivyo kuhusu jukumu la Mahakama katika jambo hili,” alieleza Vincent katika taarifa hiyo kwa umma.

Alieleza kuwa ni wazi kuwa kwa aliyetoa taarifa hizo za upotoshaji hana nia njema na mhimili wa mahakama.

“Tunaomba Watanzania na wadau wote wa mnyororo wa haki, kupuuzia taarifa hiyo na haina ukweli wowote zaidi ya nia ovu yenye lengo la kuchafua taswira ya mhimili wa Mahakama,” alisema Vincent katika taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button