Mahujaji waanza Hija Saudi Arabia

IBADA ya Hija ya kila mwaka imeanza huku umati wa Waislamu waliovalia mavazi meupe wakizunguka Kaaba, jengo lenye kitovu cha eneo takatifu la Uislamu.

Hija ya kila mwaka ilianza Jumapili huko Makka, Saudi Arabia kwa tawaf, kuzunguka Kaaba, katika tukio ambalo linatarajiwa kuvunja rekodi za mahudhurio.

“Mwaka huu, tutashuhudia Hija kubwa zaidi katika historia,” afisa katika Wizara ya Hajj na Umrah ya Saudia alisema.

Advertisement

Zaidi ya Waislamu milioni 2.5 wanatarajiwa kushiriki, kwani vizuizi vya janga la UVIKO-19 vilivyowekwa tangu 2020 vimelegezwa kikamilifu.

Mwaka huo, watu 10,000 tu waliruhusiwa kushiriki; 59,000 mwaka 2021; na mwaka jana kulikuwa na watu milioni moja.

“Ninaishi siku nzuri zaidi za maisha yangu,” Abdelazim, Mmisri mwenye umri wa miaka 65 ambaye aliweka akiba kwa miaka 20 kulipa gharama ya dola za Marekani 6000 (Sh milioni 14.

4) alizohitaji kuhudhuria ibada hiyo, aliliambia shirika la habari la AFP kwenye tovuti hiyo.

Siku ya Jumapili jioni, mahujaji waliaanza safari yao kuelekea Mina, takriban kilomita 8 kutoka al-Masjid al-Haram ya Meka, au Msikiti Mkuu, kabla ya kukusanyika kwenye Mlima Arafat, ambapo Mtume Muhammad anaaminika kuwa alifanya mahubiri ya mwisho.