DAR ES SALAAM: Mrembo machachari na msanii wa Bongo Fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ anatarajia kuzindua kipindi cha luninga kitakachoonesha maisha yake halisi ‘Reality Show’.
Tukio hilo linatarajiwa kufanyika leo Alhamisi katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam.
Soma: Omondi amkalia kooni Diamond chanzo Tanasha
‘Shoo’ hiyo ya maisha halisi ya Gigy itakayoyaanika maisha ya familia na marafiki wanaomzunguka itarushwa mubashara kupitia Zamaradi TV.
Katika ‘show’ hiyo mashabiki wanatarajia kushuhudia maisha ya mama mzazi wa msanii huyo pamoja na mwanaume Mayra na dada na wadogo zake.