Majaji sita waula…

RAIS  Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa majaji sita wa Mahakama ya Rufaa.

Taarifa  ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus iliyotolewa leo Mei 18, 2023 imesema  Rais Samia amemteua Jaji Zainab Muruke, kabla ya uteuzi alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi Temeke.

Pia, amemteua Jaji Benhajj Masoud kuwa Jiaji wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria.

Advertisement

Wengine walioteuliwa ni Jaji Amour Said Khamis kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Jaji Leila Edith Mgonya, kabla ya uteuzi huo Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es Salaam.

Aidha, amemteua , Jaji Gerson Mdemu aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na Agnes Zephania Mgeyekwa aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mhakama Kuu Divishen ya Ardhi.

Taarifa ya Zuhura inasema kuwa uteuzi huo umeanza tangu Aprili 28, 2023 na uapisho wao utatangazwa muda wowote kuanzia leo.

 

 

 

 

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *