Majaji wapigwa msasa Dar

DAR ES SALAAM: MAJAJI kutoka Afrika Mashariki wamekutana leo Oktoba 20, 2023 jijini Dar es salaam kwenye mafunzo yaliyohudhuriwa na majaji mbalimbali wa Tanzania .

Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania kitengo cha ardhi, Isaya Arufani amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha na kuwafundisha majaji kuhusiana na utawala bora juu ya masuala ya sheria.

Aidha, jaji Arufani amesema Wananchi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na wapi wapeleke kesi zao.

Jaji Rais wa Afrika Mashariki, Nestor Kayobora amesema tangu mahakama ianzishwe kwa upande wa Kanda Arusha imepokea zaidi kesi mia saba (700) na mpaka sasa wanakesi zaidi 270 kwa mahakama ya awali.

Upande wa Jaji wa Mahakama Kuu kitengo cha Mkuu wa Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Godfrey Isaya amesema kutokana na mafunzo hayo wamejifunza mengi zaidi kwa upande wa uchumi na utawala bora.

Aidha mshiriki wa mafunzo hayo Mary kallomo Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu Masijala amesema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa hasa kujua kwaupana sheria na kwa ukubwa wake.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button