Majaliwa aagiza wanunuzi waliokopa tumbaku wawajibishwe

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza wanunuzi wote waliochukua tumbaku za wakulima na hawajawalipa fedha wachukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufi kishwa mahakamani kwani serikali inataka kuona wakulima wakinufaika na zao hilo. Alitoa agizo hilo jana akizungumza na viongozi wa vyama vikuu vya ushirika (AMCOS) na wakulima wa tumbaku kutoka wilaya za Urambo na Kaliua mkoani Tabora.

“Tumbaku katika Mkoa wa Tabora ni uchumi, hivyo viongozi kuanzia ngazi ya wizara, mkoa, wilaya, kata na hata vijiji simamieni ushirika kwenye maeneo yenu, ushirika ni uchumi. Sote tuwajibike kwa pamoja, tuhakikishe ushirika unapata mafanikio,” alisema.

Majaliwa alisema serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan haitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kuhujumu ushirika nchini kwa sababu imedhamiria kuuboresha. Aliwaagiza viongozi wa vyama vikuu vya ushirika waende kwa wakulima na kushirikiana nao kutatua matatizo yao.

“Kutaneni na viongozi wa mkoa na wilaya na muwaeleze changamoto zenu, viongozi wa serikali nanyi wapokeeni na muwasikilize.”

Pia, Majaliwa aliwataka viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya kijiji wasimamie mwenendo wa ushirika katika maeneo yao na wahakikishe hakuna migogoro, wizi wala dhuluma kwa wakulima.

Majaliwa alisema kitendo cha viongozi wa AMCOS kwenda kwa Waziri Mkuu na kuwasilisha kero zao wakati katika maeneo yao kuna viongozi, kinaonesha kuna shida. Alisisitiza viongozi wa halmashauri kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha maofisa ushirika nchini kukamilisha agizo lake alilolitoa mwaka jana la kuandaa kanzidata ya wakulima ili kuiwezesha serikali kuwatambua wakulima na kurahisisha utoaji huduma.

Majaliwa alisema Rais Samia anaifahamu vizuri sekta ya kilimo, ndiyo maana alifanya maboresho makubwa kwenye sekta hiyo na kuongeza viongozi wa vyama vya ushirika wahakikishe wanakutana na wakulima mara kwa mara ili kutatua kero zao.

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima wa zao la tumbaku waliozungumza kwenye mkutano huo walimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea ambayo imewasaidia kuongeza tija katika kilimo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x