LINDI: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi na wizara zote kutenga fungu ili kulipia matangazo yanayopelekwa katika vyombo vya habari na kuyaepuka madeni yanayoathiri vyombo hivyo na maslahi ya wanahabari.
Ameagiza hayo leo akiwa mkoani Lindi katika Mkutano Mkuu wa Saba wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kukemea vikali taasisi zinazokwamisha uendeshaji wa vyombo vya habari.
Ameitaka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tenkolojia ya habari kushughulikia kwa haraka changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuboresha njia za utendaji wake.
“Wekeni utaratibu wa kudumu na endelevu wa kutatua changamoto ya kudaidai. Wizara haiwezi kufanya kazi kimya, watanzania lazima wajue nini kinafanyika. Tenga bajeti ya kutosha na tuache kukopakopa wanahabari.” Amesema Waziri Mkuu.