Majaliwa aikubali Smartwasomi
TANGA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa SMARTWASOMI italeta kasi ya utekelezaji wa mpango wa serikali katika matumizi ya TEHAMA kwenye ufundishaji na pia kutatua changamoto ya uhaba wa walimu.
Alisema kuwa anaipongeza Airtel Tanzania kwa ubunifu wa suluhisho hili kwa ajili shule zetu kwani aina ya ubunifu ambao unaleta mabadiliko kwenye jamii.
Kupitia mradi huu walimu wataunganishwa na maktaba ya mtandao ambapo watapata majarida, vitabu na vitendea kazi vyote vya kufundishia na kusomea bure bila gharama yoyote ile.
Nafahamu kuwa walishapatiwa vishkwambi hivyo sina shaka kuwa watatumia maktaba hizo za mtandao kikamilifu.
Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh alisema kuwa amekuwa akitafakari juu ya dhamira ya muda mrefu ya kampuni hiyo katika elimu ya kidijitali tangu mwaka 2015 wakati uzinduzi wa VSOMO kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) – jukwaa la simu kuwezesha upatikanaji wa kozi ya VETA bila kuwa na hitaji la kuhudhuria darasani kimwili.