Majaliwa akaribisha wawekezaji kwenye  mbolea

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaalika wawekezaji waliobobea kwenye sekta ya mbolea ili waje kufungua viwanda vya mbolea nchini.

Ametoa mwaliko huo leo Alhamisi, Julai 27, 2023, wakati akizungumza kwenye mjadala uliohusu Uimarishaji wa Soko la Mbolea kama njia ya kuondoa njaa barani Afrika uliofanyika kwenye kituo cha mikutano na maonesho cha Expo Forum, jijini St. Petersburg, Urusi. 

Amesema uamuzi wa Rais Dk  Samia Suluhu Hassan wa kuongeza bajeti ya kilimo una nia ya kuifanya Tanzania iwe eneo la uzalishaji la kulisha Afrika Mashariki, SADC na bara zima la Afrika. 

“Bado tuna changamoto ya upatikanaji wa mbolea kwa sababu ikikosekana inaathiri uzalishaji wa chakula. 

“Mbolea kwa sasa ndiyo msingi wa uzalishaji chakula. Uzalishaji wetu unatumia zaidi ya asilimia 80 na kwa maana hiyo tunalazimika kutumia fedha nyingi ili kuagiza mbolea kutoka nje na msisitizo wa sasa ni kuzalisha mbolea yetu. 

“Tunatumia fursa hii kutafuta marafiki ambao wako tayari kuja kuwekeza kwenye mbolea. Mahitaji yetu ni zaidi ya tani 800,000 wakati uzalishaji wetu ni tani 200,000. Tumeshapata kiwanda ambacho kinazalisha mbolea na sasa wameshafikisha tani 400,000 na wanalenga kufikia tani 800,000 lakini hatuwezi kutegemea kiwanda kimoja peke yake,” amesema. 

Amesema Tanzania ina rasilimali ya gesi ambayo inaweza kutumika kutengeneza mbolea ukiacha zile za kawaida za wanyama. 

“Tukifanikiwa kuongeza uzalishaji wa mbolea, tutakuwa na nafasi ya kuzalisha chakula zaidi. Jukwaa hili ni nafasi pekee ya kualika wawekezaji waliobobea kwenye maeneo kama haya,” amesisitiza. 

Mapema, Waziri Mkuu alishiriki Jukwaa la Kimataifa la Uchumi na Kibinadamu lililofunguliwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwenye kituo cha mikutano na maonesho cha Expo Forum, jijini St. Petersburg, Urusi.

Jukwaa hilo ambalo limehudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Umoja wa Afrika wakiwemo wa Uganda, Msumbiji, Zimbabwe, Sudan, limehusisha pia Mawaziri, wakuu wa Mashirika ya Kikanda, Taasisi na Mashirika ya kiserikali kutoka Urusi na Afrika.

Jukwaa hilo linaenda sambamba na maonesho ya kimataifa ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka Urusi na Afrika pamoja na majukwaa ya majadiliano (side meetings) zaidi ya 30 ambayo yanahususu mada mbalimbali zikiwemo za masuala ya vijana, kilimo, afya, elimu, masuala ya kibinadamu. 

Baadhi Mawaziri na Makatibu Wakuu na wakuu wa taasisi kutoka Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanashiriki majukwaa hayo ya majadiliano.

Maudhui makuu ya jukwaa hilo linalotarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania na mataifa mengine ya Afrika kushirikiana na Urusi kukuza uchumi, kutafuta ushirikiano wa kibiashara na kushughulikia changamoto za kimaendeleo yanahusu Uchumi Mpya wa Dunia (the New Global Economy); Usalama Jumuishi (Integrated Security); Sayansi na Teknolojia (Science and Technology); na Masuala ya Kibinadamu na Kijamii (Humanitarian Issues).

Kesho Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi, kwa niaba ya Rais Dk  Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Christy R. Miller
Christy R. Miller
1 month ago

I am making really good money (80$ to 100$ / hr. )online from my laptop. I was greatly surprised at the same time as my neighbour advised me she changed into averaging $100 however I see the way it works now. sd370 I experience mass freedom now that I’m my non-public boss.
Everybody should start earning money online by
.
.
using this website____ https://Fastinccome.blogspot.Com/

Last edited 1 month ago by Christy R. Miller
gajigif330
gajigif330
Reply to  Christy R. Miller
1 month ago

Making an extra $15,000 per month from home by doing easy copy and paste type internet work. I earned $18,000 from this simple at-home job. Everyone may now easily generate additional money online working
.
.

Detail Here———————> >> https://newjobshiring.blogspot.com/

Last edited 1 month ago by gajigif330
Hudson Leigh
Hudson Leigh
Reply to  gajigif330
1 month ago

I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $35k a month doing this and she convinced me to try.For Details
.
.
For Details►—————————➤ https://Www.Coins71.Com

Last edited 1 month ago by Hudson Leigh
gajigif330
gajigif330
Reply to  Christy R. Miller
1 month ago

Making an extra $15,000 per month from home by doing easy copy and paste type internet work. I earned $18,000 from this simple at-home job. Everyone may now easily generate additional money online working

Detail Here———————> >> https://julizaah9.blogspot.com/

Last edited 1 month ago by gajigif330
Asonna
Asonna
1 month ago

> Welcome to the best sex dating site — https://ok.me/wqPA1

Julia
Julia
1 month ago

Making extra salary every month from house more than $15,000 just by doing simple copy and paste like online job. I have received $18,000 from this easy home job. Everybody can now makes extra cash online easily.
.
.
Detail Here———————————————–>>>  http://Www.OnlineCash1.Com

tacem
1 month ago

My last month paycheck was for 11000 dollars… All i did was simple online work from comfort at home for 3-4 hours/day that I got from this agency I discovered over the internet and they paid me for it 95 bucks every hour…..>info on web–
 https://www.pay.salary49.com

Back to top button
7
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x