WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amefika Kariakoo kuzungumza na Jumuiya ya wafanyabiashara wa soko hilo, badala ya Mei 17, 2023 kama ofisi yake ilivyotoa taarifa hapo awali.
–
Majaliwa amefika eneo hilo kuzungumza kuhusu mgomo wa wafanyabiashara hao pamoja na kero zinazowasumbua
–
Asubuhi ya leo wafanyabiashara hao waligoma kufungua maduka kwa madai ya utitiri wa kodi na tozo walizodai kutokuwa rafiki.
–
Taarifa ya awali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa Majaliwa alipanga kukutana na uongozi wa jumuiya hiyo katika ukumbi wa Anatouglou uliopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
–


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Add a comment